Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 1

Al-Anbiyaa 21:1

الأنبياء

ٱقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِى غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ

Maana

Imewakaribia watu hesabu yao, nao wako katika kughafilika wanapuuza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanapuuza. [1]

[1] Umewakaribia washirikina wakati wao wa kuhisabiwa Siku ya Kiyama, nao hali wameghafilika na kitisho chake, wanapuuza kuiamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Umekaribia wakati wa kuhesabiwa watu juu ya matendo waliyoyatanguliza, pamoja na hivyo, makafiri wanaishi wakiwa kwenye hali ya kupumbaa, wameghafilika na uhakika huu, wakiwa kwenye hali ya kulipa mgongo onyo hili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net