Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 20 · Aya ya 86

Taa-Haa 20:86

طه

فَرَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوْمِهِۦ غَضْبَـٰنَ أَسِفًا ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ أَلَمْ يَعِدْكُمْ رَبُّكُمْ وَعْدًا حَسَنًا ۚ أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ ٱلْعَهْدُ أَمْ أَرَدتُّمْ أَن يَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَخْلَفْتُم مَّوْعِدِى

Maana

Basi Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakuwaahidi ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ghadhabu ya Mola wenu Mlezi iwashukie, ndiyo maana mkavunja miadi yangu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi yangu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo Mûsã akarudi kwa watu wake akiwa ni mwenye hasira na masikitiko na akawaambia, Enyi watu wangu, Si Allah Mtukufu Amewaagiza agizo zuri la kuiteremsha Taurati? Kwani hiyo ahadi imepitiwa na kipindi kirefu mkaona kuwa agizo limechelewa au mlitaka kufanya jambo ambalo kwalo zitawashukia hasira kutoka kwa Mola wenu ndipo mkaenda kinyume na agizo langu nililowaahidi, mkaabudu ndama na mkaacha kujilazimisha na amri zangu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Taa-Haa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net