Taa-Haa 20:76
طهجَنَّـٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ مَن تَزَكَّىٰ
Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ndiyo malipo ya mwenye kujitakasa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
katika mabustani ya Pepo ya kukaa daima ambayo mito inapita chini ya miti yake, wakiwa ni wenye kukaa humo milele. Neema hiyo ya daima ni malipo kutoka kwa Allah Mtukufu kwa mwenye kujisafisha nafsi yake na uchafu, uovu na ushirikina, na akamuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, akamtii na akajiepusha na matendo ya kumuasi na akakutana na Mola wake na huku hamshirikishi yoyote kati ya viumbe Vyake katika kumuabudu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net