Taa-Haa 20:72
طهقَالُوا۟ لَن نُّؤْثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَآءَنَا مِنَ ٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلَّذِى فَطَرَنَا ۖ فَٱقْضِ مَآ أَنتَ قَاضٍ ۖ إِنَّمَا تَقْضِى هَـٰذِهِ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَآ
Wakasema: Hatutakupendelea wewe kuliko ishara waziwazi zilizotujia, na kuliko yule aliyetuumba. Basi hukumu utavyohukumu; kwani wewe hakika unahukumu tu haya ya maisha ya duniani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya maisha ya duniani tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wachawi wakasema kumwambia Fir‛awn, Hatutakutanguliza wewe tukakusikiliza na tukaifuata dini yako juu ya yale aliyotuletea Mûsã yaliyo waziwazi yanayojulisha ukweli wake na ulazima wa kumfuata na kumtii Mola wake. Na hatutautanguliza umola wako wa kujipangia juu ya umola wa Allah Mtukufu Aliyetuumba. Basi fanya kile utakachotufanya. Ukweli ni kwamba utawala wako ni hapa katika maisha ya duniani. Na utakachokifanya kwetu si kitu isipokuwa ni adhabu itakayokoma kwa kukoma dunia hii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net