Taa-Haa 20:123
طهقَالَ ٱهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًۢا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّى هُدًى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَاىَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ
Akasema: Ondokeni humo nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uongofu kutoka kwangu basi atakayeufuata uongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Akamwambia Ãdam na Hawâ’ Shukeni kutoka kwenye Pepo muende ardhini nyote pamoja na Iblisi, kwani nyinyi na yeye ni maadui. Mtakapojiwa na uongofu na maelezo kutoka kwangu, basi mwenye kufuata uongofu wangu na maelezo yangu na akayatumia yote mawili, yeye atakuwa amefuata usawa duniani na ataongoka, na hatasumbuka huko Akhera kwa kuteswa na Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net