Al-Baqara 2:72
البقرةوَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَٱدَّٰرَْٰٔتُمْ فِيهَا ۖ وَٱللَّهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ
Na mlipomuua mtu, kisha mkahitilafiana kwayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mlipo muuwa mtu, kisha mkakhitalifiana kwayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyo kuwa mkiyaficha. [72]
[72] Na kumbukeni siku mlipo muuwa mtu, mkakhasimiana wenyewe kwa wenyewe, mkautetea ukhalifu, mkawa mkituhumiana kwa mauwaji, na hali Mwenyezi Mungu anaijua hakika, na ataikashifu na kuidhihirisha juu ya kuificha kwenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Kumbukeni, mlipomuua mtu, mkabishana kuhusu yeye, akawa kila mmoja ajiepushia nafsi yake tuhuma ya kuua na hali Allah Mtukufu ni Mwenye kuyafichua yale ambayo mlikuwa mkiyaficha kuhusu kifo cha yule aliyeuawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net