Al-Baqara 2:200
البقرةفَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَـٰسِكَكُمْ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَذِكْرِكُمْ ءَابَآءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِى ٱلدُّنْيَا وَمَا لَهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ مِنْ خَلَـٰقٍ
Na mkishatimiza ibada zenu za Hija, mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu au utajo mkubwa zaidi. Na katika watu kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani!” Naye katika Akhera hana fungu lolote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkisha timiza ibada zenu basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyo kuwa mkiwataja baba zenu au mtajeni zaidi. Na wapo baadhi ya watu wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani! Naye katika Akhera hana sehemu yoyote. [200]
[200] Mkisha maliza a'mali za Hija na ibada zake wacheni mliyo kuwa mkiyafanya zama za ujahili ya kutafakhari kwa baba zenu na kukumbusha mambo yao, bali makumbusho yenu na kutukuza kwenu kuwe kwa Mwenyezi Mungu kama mlivyo kuwa mkiwakumbuka baba zenu, bali mtajeni Yeye kwa wingi zaidi kuliko wazee wenu, kwani Yeye ndiye Mwenye kuzitawala neema zenu na neema za baba zenu vile vile. Na humu mwahali mwa Hija ndio khasa mwahala mwa dua na kuombea fadhila na kheri na rehema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu. Na walikuwako baadhi ya Mahujaji wakifupiza dua zao kwa mambo na kheri za dunia tu. Hao hawapati sehemu yoyote ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mtakapokamilisha ibada yenu na mkamaliza amali zenu za Hija, mtajeni Allah Mtukufu na mumsifu kwa wingi kama vile mnavyotaja fahari za wazee wenu na zaidi ya hivyo. Kwani wamo miongoni mwa watu kikundi ambacho hima yao yote ni dunia. Hapo, wao huomba wakisema, «Ewe Mola wetu, tupe duniani afya, mali na wana.» Hao hawana Akhera hisa wala fungu lolote, kwa kuipuza Akhera na kujishughulisha na dunia tu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net