Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 18

Al-Baqara 2:18

البقرة

صُمٌّۢ بُكْمٌ عُمْىٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ

Maana

Ni viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.[1]

[1] Ni viziwi kwa sababu hawaisikii heri. Ni mabubu kwa sababu hawaitamki heri. Na ni vipofu kwa sababu hawaioni haki. Kwa hivyo, hawatarejea katika haki kwa kuwa waliiacha baada ya kuijua. Tofauti na mwenye kuiacha haki kwa ujinga na upotovu, yeye yuko karibu zaidi na kurudi katika haki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. [18]

[18] Watu hawa ni kama viziwi, kwani wamepoteza manufaa ya kusikia; hawaisikii Haki kwa msikio wa kuikubali na kuitikia. Nao ni kama bubu, kwa sababu hawatamki la uwongofu au la Haki. Na wao kama vipofu, kwani hawanufaiki kwa macho yao. Hawazingatii na kujikataza. Basi hao hawaachi upotovu wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wao ni viziwi, hawaisikii haki kwa kuizingatia, ni mabubu, hawaitamki haki, ni vipofu, hawauoni mwangaza wa uongofu. Kwa hivyo, hawawezi kurudi kwenye Imani ambayo waliiacha na kuchukuwa upotevu badali yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net