Al-Baqara 2:175
البقرةأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلضَّلَـٰلَةَ بِٱلْهُدَىٰ وَٱلْعَذَابَ بِٱلْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَآ أَصْبَرَهُمْ عَلَى ٱلنَّارِ
Hao ndio walionunua upotovu kwa uongofu, na adhabu kwa msamaha. Basi ni wavumilivu wa namna gani hawa kwa Moto!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio walio nunua upotofu badala ya uwongofu, na adhabu badala ya maghfira. Ama wavumilivu wa Moto watu hawa! [175]
[175] Hao ndio wenye madhambi walio khiari upotovu wakaacha uwongofu, na kwa hivyo wakastahiki adhabu ya Akhera badala ya kupata msamaha. Watakuwa kama mwenye kununua baat'ili kwa haki, na chenye upotovu kwa chenye uwongofu. Hakika hali yao ni ya kustaajabisha, kwa kuwa wanavumilia kufanya mambo ambayo hayana budi kuwapelekea kwenye adhabu, na tena wakawa wenyewe wakayaonea uzuri hayo yanayo wapeleka huko!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao wanaosifika na sifa hizi wamechagua upotevu wakaacha uongofu, na wakachagua adhabu ya Allah Mtukufu wakaacha msamaha wake. Ni ujasiri ulioje wao wa kuchagua Moto kwa kufanya vitendo vya watu wa Motoni! Anastaajabu Allah Mtukufu kwa kujitokeza kwao kulifanya hilo. Basi oneni ajabu, enyi watu, juu ya ujasiri wao na uvumilivu wao kwenye Moto na kukaa kwao humo. Maneno haya yametumika kwa njia ya kuwadhalilisha na kuwachezea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net