Al-Baqara 2:173
البقرةإِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيْرِ ٱللَّهِ ۖ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Hakika Yeye amekuharamishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [173]
[173] Sio yaliyo harimishwa wanayo zua Washirikina na Mayahudi. Lakini mlicho harimishiwa nyinyi Waumini ni nyamafu, mzoga, yaani mnyama asiye chinjwa, na mfano wake katika kuharimishwa ni nyama ya nguruwe, na nyama ambaye wakati wa kuchinjwa ametajiwa jina lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu, kama vile miungu ya uwongo au mfano wake. Juu ya hivyo mtu akilazimika kwa dharura kula kidogo katika vilivyo katazwa kwa ajili ya njaa, na hakupata kinginecho, au kwa kulazimishwa, basi hana makosa juu yake. Lakini ajitenge na mwendo wa kijaahili, kutaka kula vilivyo katazwa kwa kutamani tu, na wala asipite kiasi kula kuliko cha kuondoa njaa tu. Hali ya dharura inaruhusisha kinacho harimishwa, kwa sababu mauti ya yakini yanashinda madhara yanayo weza kustahamilika, na kwamba mwenye kulazimika kwa dharura haimfalii kupindukia mpaka wa dharura, wala asikiuke kile alicho lazimika kukila.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Amewaharamishia nyinyi kinachowadhuru, kama mfu ambaye hakuchinjwa kwa njia ya kisheria, na damu inayotiririka, na nyama ya nguruwe, na vichinjwa ambavyo vilikusudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu. Na katika wema wa Allah Mtukufu na usahilishaji Wake kwenu ni kwamba Amewahalalishia nyinyi kuvila vitu hivi vilivyoharamishwa wakati wa dharura. Hivyo basi, yoyote ambaye dharura ilimpelekea kula kitu katika hivyo, pasi na kuwa ni mwenye kudhulumu katika kula kwake kwa kupitisha kipimo cha haja yake, wala kuikiuka mipaka ya Allah Mtukufu katika yale aliyohalalishiwa, basi huyo hana dhambi kwa hilo. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net