Al-Baqara 2:138
البقرةصِبْغَةَ ٱللَّهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ ٱللَّهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُۥ عَـٰبِدُونَ
Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu. Na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu. [138]
[138] Waambieni: Hakika Mwenyezi Mungu ametuongoa sisi kwa uwongofu wake mwenyewe, na ametuonyesha hoja zake. Na hapana mbora zaidi kwa uwongofu na hoja kuliko Mwenyezi Mungu. Na sisi hatumnyenyekei ila Mwenyezi Mungu. Na wala hatufuati ila anavyo tuongoa na kutuongoza Yeye. (Hilo ndilo pambo, au batizo, au kutia rangi kwa Mwenyezi Mungu--S'ibghatu Llahi).
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Jilazimisheni na Dini ya Allah Mtukufu ambayo Ameifanya inasibiane na maumbile yenu. Kwani hakuna maumbile mazuri kuliko yale ambayo Allah Mtukufu Amewaumbia watu. Jilazimisheni nayo na mseme, “Sisi ni wenye kuifuata, ni watiifu kwa Mola wetu katika kufuata kwetu mila ya Ibrãhîm.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net