Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 134

Al-Baqara 2:134

البقرة

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْـَٔلُونَ عَمَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Hao ni watu waliokwishapita. Watapata waliyoyachuma, nanyi mtapata mtakayoyachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyokuwa wakiyafanya wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao. [134]

[134] Tena imekuwaje enyi Mayahudi kujadili mambo ya watu hawa? Hao ni watu walio kwisha pita na njia yao. Tena wao peke yao watavuna yale waliyo yatenda katika maisha yao. Nyinyi, basi, hamtaulizwa kitu juu ya vitendo vyao, na wala nyinyi hamtapata faida yoyote katika hayo. Nanyi hamtavuna ila yale matunda ya vitendo vyenu mnavyo vitenda nyinyi wenyewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ni Ummah waliopita miongoni mwa wale waliowatangulia nyinyi. Wao wana amali zao, na nyinyi muna amali zenu. Wala hamtaulizwa kuhusu amali zao. Na wao hawataulizwa kuhusu amali zenu. Na kila mmoja atalipwa kulingana na aliyoyatenda. Mtu hateswi kwa kosa la yoyote mwengine. Na haimnufaishi mtu ila Imani yake na uchaji Mungu wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net