Maryam 19:9
مريمقَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَىَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْـًٔا
Akasema: Hivyo ndivyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwishakuumba wewe zamani na wala hukuwa kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Malaika akasema kumjibu Zakariyyã juu ya kile alichokionea ajabu, «Mambo ni kama unavyosema kuwa mke wako ni tasa na kuwa wewe umefikia upeo wa uzee, lakini Mola wako Amesema, ‘Kumuumba Yahyã kwa namna hii ni jambo sahali na jepesi kwangu.’» Kisha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Alimtajia Zakariyyã jambo la ajabu zaidi kuliko lile aliloliuliza akasema, «Na nimekuumba wewe kabla ya Yahyã na hukuwa ni kitu chenye kutajika wala kilichoko».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net