Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 19 · Aya ya 82

Maryam 19:82

مريم

كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا

Maana

Sivyo hivyo! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mambo sivyo kama wanavyodai. Hawa waungu hawatakuwa ni nguvu kwao, lakini waungu hawa watawaruka huko Akhera kuwa waliwaabudu wao na watakuwa ni wenye kusaidia katika kuteta na wao na kuwakanusha, kinyume na vile walivyodhania juu yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Maryam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net