Maryam 19:79
مريمكَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُۥ مِنَ ٱلْعَذَابِ مَدًّا
Hasha! Tutaandika anayoyasema, na tutamuongezea sawasawa katika adhabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hasha! Tutaandika anayo yasema, tutamkunjulia muda wa adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mambo siyo kama vile alivyodai yule kafiri, kwani yeye hana ujuzi wala hakupewa ahadi. Tutatayaandika anayoyasema ya urongo na uzushi juu ya Allah Mtukufu, na huko Akhera tutamuongezea aina mbali mbali za mateso, kama alivyojiongezea upotovu na upotevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net