Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 19 · Aya ya 76

Maryam 19:76

مريم

وَيَزِيدُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱهْتَدَوْا۟ هُدًى ۗ وَٱلْبَـٰقِيَـٰتُ ٱلصَّـٰلِحَـٰتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا

Maana

Na Mwenyezi Mungu huwazidishia wale walioongoka uongofu. Na mema yenye kubakia ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana marejeo mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu. Na mema yenye kudumu ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anawaongezea waja Wake, walioongoka katika dini Yake, uongofu juu ya uongofu walionao kwa yale yanayowapitia mara kwa mara ya kuyaamini malazimisho ya Allah Mtukufu na kuyafuata kivitendo. Na matendo mema yaliyosalia yana malipo bora kwa Allah Mtukufu kesho Akhera, na yana matokeo bora na mwisho mwema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Maryam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net