Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 19 · Aya ya 71

Maryam 19:71

مريم

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا

Maana

Wala hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa ataifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuna katika nyinyi, enyi watu, yoyote isipokuwa ataufikia huo Moto kwa kupita juu Ṣirâṭ (Njia) iliyotandikwa juu ya daraja la moto wa Jahanamu, kila mmoja kulingana na matendo yake. Hilo ni jambo lenye kuwa kwa lazima, Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Amepitisha na Ameamua kwamba halina budi kuwa, hakuna namna ya kuliepuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Maryam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net