Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 19 · Aya ya 46

Maryam 19:46

مريم

قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ ءَالِهَتِى يَـٰٓإِبْرَٰهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَٱهْجُرْنِى مَلِيًّا

Maana

(Baba) akasema: Je huitaki miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali kwa muda mrefu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali kwa muda!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Baba yake Ibrãhîm akasema kumwambia mwanawe, Kwani wewe umegeuka na kukataa kuabudu waungu wangu, ewe Ibrãhîm Basi usipokomeka kuwatukana, nitakuua kwa kukupiga mawe. Na niondokee, usikutane na mimi wala usiseme na mimi kwa kipindi cha muda mrefu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Maryam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net