Maryam 19:12
مريميَـٰيَحْيَىٰ خُذِ ٱلْكِتَـٰبَ بِقُوَّةٍ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْحُكْمَ صَبِيًّا
Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hekima angali mtoto.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipozaliwa Yahyã na akafikia umri wa kufahamu maneno, Allah Mtukufu Alimuamuru aichukue Taurati kwa bidii na jitihada kwa kusema, «Ewe Yahyã! Ichukue Taurati kwa bidii na jitihada kwa kuyahifadhi matamko yake na kuyafahamu maneno yake na kuitumia, na tulimpa busara na ufahamu mzuri ilhali yeye ni mdogo wa miaka».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net