Al-Kahf 18:90
الكهفحَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ ٱلشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَىٰ قَوْمٍ لَّمْ نَجْعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتْرًا
Hata alipofika machomozeo ya jua, akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu tusio wawekea pazia la kuwakinga nalo. [90]
[90] Hata akafika linapo chomoza jua, kwa ionekanavyo kwa macho, mwisho wa majenzi. Akawaona watu wanaishi katika ushenzi kabisa. Hawana hata cha kuwasitiri na joto.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mpaka alipofika upande wa kutoka jua alilikuta hilo jua linawatokea watu wasiokuwa na majengo ya kuwasitiri wala miti ya kuwapatia kivuli cha kuwakinga na jua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net