Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 86

Al-Kahf 18:86

الكهف

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ ٱلشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِى عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ قُلْنَا يَـٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا

Maana

Mpaka alipofika machweo ya jua, akaliona linatua katika chemichemi yenye matope meusi. Na pale akawakuta kaumu fulani. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu au uwafanyie uzuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema. [86]

[86] Akenda mpaka akafika pahala mbali huko upande wa magharibi, akalikuta jua kwa linavyo onekana kwa macho kama kwamba linazama pahala penye chemchem ya maji ya moto na matope meusi. Na karibu ya chemchem hii Dhul- Qarnaini aliwakuta watu makafiri. Mwenyezi Mungu akamtia moyoni mwake afanye mojapo ya mambo mawili: Ama awaite kwenye Imani, na hili kwa hakika ni jambo zuri; au awapige vita ikiwa hawakuitikia wito wa Imani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mpaka alipofika Dhulqarnain upande wa jua la kuchwa, alilikuta jua kwa vile alivyoliona kana kwamba linakuchwa ndani ya chemchemu ya maji moto yenye udongo mweusi, na akawakuta watu upande huo wa jua la kuchwa. Tulisema, «Ewe Dhulqarnain! Ima uwaadhibu kwa kuwaua au kwa linginelo, iwapo hawatakubali upweke wa Allah Mtukufu au uwatendee wema uwafundishe uongofu na uwaonyeshe usawa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net