Al-Kahf 18:74
الكهففَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَـٰمًا فَقَتَلَهُۥ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةًۢ بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْـًٔا نُّكْرًا
Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuua. (Musa) akasema: Ala! Umemuua mtu asiye na kosa, na wala hakuua nafsi yoyote! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuuwa. (Musa) akasema: Ala! Umemuuwa mtu asiye na kosa, na wala hakuuwa! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa! [74]
[74] Na baada ya kutoka kwenye jahazi ile wakaingia kuendelea na safari yao. Njiani wakamkuta kijana. Yule mja mwema akamuuwa yule kijana! Musa akasema kwa kuchukia: Unakwenda muuwa mtu asiye na kosa lolote, na wala hakumuuwa mtu yeyote? Hakika umefanya jambo ovu kweli kweli!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Al-Khiḓr akakubali udhuru wake. Kisha wakatoka mashuani, na walipokuwa wanatembea kwenye ufuo wa pwani, ghafla wakamuona kijana yuwacheza na wenzake, na Al- Khiḓr akamuua. Mūsă akamlaumu kwa nguvu na akasema, «vipi umeiua nafsi safi isiyokuwa na kosa, isiyofikia umri wa kubeba majukumu, na haijaua mtu mpaka istahili kuuawa? Kwa hakika umefanya jambo baya sana».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net