Al-Kahf 18:7
الكهفإِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى ٱلْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا
Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika tumevifanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao wenye vitendo vizuri zaidi. [7]
[7] Sisi tumewaumba kwa kheri na shari, na tumevifanya vilio juu ya ardhi ni pambo lake kwa ajili ya manufaa ya watu wake. Hivyo tunawatendea vitendo kama ni mtihani wapate kudhihiri kati yao wenye a'mali njema. Basi aliye pumbazwa na ulimwengu, na asiishughulikie Akhera, huwa amepotea. Na aliye iamini Akhera, huyo huwa ameongoka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika sisi tumevifanya vilivyoko juu ya uso wa ardhi viwe ni pambo lake na ni manufaa kwa watu wake, ili tuwatahini ni nani kati yao aliye mzuri zaidi wa vitendo vya utiifu kwetu na ni nani kati yao aliye mbaya zaidi wa kufanya maasia, na tutamlipa kila mtu anachostahiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net