Al-Kahf 18:17
الكهفوَتَرَى ٱلشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَٰوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ ٱلْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَهُمْ فِى فَجْوَةٍ مِّنْهُ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ ۗ مَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ وَلِيًّا مُّرْشِدًا
Na unaliona jua linapochomoza, linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni, na linapokuchwa, linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi huyo ameongoka. Na yule ambaye anampoteza, basi hutampatia msimamizi wa kumwongoza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na unaliona jua linapo chomoza linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa basi huyo ni mwenye kuongoka. Na anaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi. [17]
[17] Na lile pango lilikuwa kwenye mlima, lina nafasi ndani. Lilielekea kaskazini, linapigwa na upepo mzuri. Jua likichomoza muanga wake huwa kuliani mwao, na miale yake huwa mbali nao; na likichwa huwa kushotoni mwao. Kwa hivyo lile jua halipigi ndani ya pango, na kwa hivyo walisalimika na joto la jua, na upepo wa kaskazi unawaingilia. Na yote hayo ni katika ishara za kudra ya Mwenyezi Mungu. Na anaye pata tawfiki ya Mwenyezi Mungu kuokoka basi huokoka, na aliye kosa tawfiki hatopata wa kumwongoa baada yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walipofanya hivyo, Allah Mtukufu Aliwatia usingizi wakalala na Akawahifadhi. Na utaliona jua, ewe mwenye kuwatazama wao, linapochomoza upande wa mashariki linapenyeza pale walipo upande wa kulia, na linapozama linawaacha upande wa kushoto, na hali wao wako kwenye sehemu kunjufu ndani ya pango, joto la jua haliwasumbui na hewa haiwakatikii. Hayo tuliyowafanyia vijana hawa ni miongoni mwa dalili za uwezo wa wa Allah Mtukufu. Basi yoyote yule ambaye Allah Mtukufu Atamuafikia kuongoka kwa aya Zake, yeye ndiye mwenye kuongoka, na yoyote ambaye Hatamuafikia hilo, hutapata yoyote wa kumsaidia na kumuongoza kuifikia haki, kwani kuafikiwa na kutoafikiwa viko mikononi mwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net