Al-Israa 17:49
الإسراءوَقَالُوٓا۟ أَءِذَا كُنَّا عِظَـٰمًا وَرُفَـٰتًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا
Na walisema: Je! Tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyovurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya? [49]
[49] Wanao kataa kuwa watafufuliwa wanasema: Hivyo tutafuliwa baada ya kwisha kuwa mafupa yaliyo bunguliwa, na mapande mbali mbali, tukawa hai na umbo jipya? Haya hayaingii akilini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Washirikina walisema wakikanusha kwamba wataumbwa umbo jipya baada ya mifupa yao kuoza na kuwa mbalimbali, «Je, sisi tutafufuliwa ufufuzi mpya Siku ya Kiyama?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net