Al-Israa 17:44
الإسراءتُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَـٰوَٰتُ ٱلسَّبْعُ وَٱلْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَىْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِۦ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا
Zinamtakasa mbingu zote saba na ardhi na vyote vilivyo ndani yake. Na hakuna kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira. [44]
[44] Hakika mbingu saba na ardhi, na viumbe vyote viliomo humo, vinamtakasa na kumtukuza, na vinaonyesha uzuri wa kuumba kwake, na kutakasika kwake Subhanahu na kila upungufu, na kukamilika ufalme wake, na kwamba Yeye hana mshirika na yeyote katika viumbe wa Ufalme wake uliyo enea. Vyote hivyo vinamtakasa na kumsifu. Lakini makafiri hawafahamu hoja hizi kwa kutawaliwa nyoyo zao na mghafala. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwao, na Mwenye kuwasamehe wanao tubu. Kwa hivyo hawafanyii haraka kuwapa adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zinamtakasa Yeye, kutukuka ni Kwake, mbingu saba na ardhi na viumbe wote waliyo humo. Na kila kitu kilichoko katika ulimwengu huu kinamtakasa Allah Mtukufu Aliyetukuka na sifa za upungufu, utakaso unaofungamana na kumsifu na kumshukuru, kutukuka ni Kwake, lakini nyinyi,enyi watu, hamtambui hilo. Kwa kweli, Yeye ni Mpole kwa waja Wake, hawaharakishii adhabu wanaomuasi, ni Mwingi wa msamaha kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net