An-Nahl 16:86
النحلوَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ شُرَكَآءَهُمْ قَالُوا۟ رَبَّنَا هَـٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدْعُوا۟ مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا۟ إِلَيْهِمُ ٱلْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَـٰذِبُونَ
Na wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako." Lakini hao watawatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio shirikisha watakapo waona hao walio washirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaabudu badala yako. Ndipo wale watakapo watupia kauli:Hakika nyinyi ni waongo! [86]
[86] Na walio wafanya miungu yao washirika wa Mwenyezi Mungu na wakawaabudu watapo sema: Ewe Mola Mlezi wetu! Hawa ndio washirikishwa wetu tulio tukiwaabudu kwa makosa. Basi tupunguzie adhabu kwa kuwapa wao baadhi ya adhabu! Washirikishwa wao watajibu: Ama hakika nyinyi washirikina waongo kwa kudai kwenu kuwa sisi ni washirika wa Mwenyezi Mungu, na kwamba nyinyi mkituabudu! La kweli ni kuwa mkiabudu matamanio yenu tu, wala sisi hatukuwa washirika kama mlivyo dai. (Nabii Isa a.s. amesema: "Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu." - Injili ya Mathayo 7.21-27)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliokanusha watakapowaona Siku ya Kiyama waungu wao waliokuwa wakiwaabudu pamoja na Allah Mtukufu watasema, «Mola wetu! Hawa ndio washirika wetu tuliokuwa tukiwaabudu badala yako.» Hapo waungu hao watatamka kuwakanusha wale waliowaabudu na watasema, «Hakika nyinyi, enyi washirikina, ni warongo, mlipotufanya sisi ni washirika wa Allah Mtukufu na mkatuabudu pamoja na Yeye. Sisi hatukuwaamuru hilo, wala hatukudai kwamba sisi tunastahiki uungu, lawama ni juu yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net