Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 69

An-Nahl 16:69

النحل

ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسْلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizofanywa nyepesi kuzipita. Na kwenye matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponya kwa watu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu.Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri. [69]

[69] Kisha Subhanahu akamhidi Nyuki ale matunda ya miti na mimea mbali mbali, na akamsahilishia afuate njia alizo mtengezea Mola wake Mlezi, na akatoa kutokana na matumbo yake kinywaji, nacho ni asali, chenye rangi mbali mbali. Na hiyo asali imekuwa ni dawa ya kuwaponyesha watu. Hakika katika hayo pana ufundi wa ajabu wa kuonyesha nguvu, na kuwepo Mwenye kuumba, na Mwenye kuweza, Mwenye hikima. Wenye kutumia akili zao wananufaika kwa mazingatio hayo, na watapata furaha ya daima. Asali ya nyuki ni mchanganyiko wa glucose na livulose, nayo ni namna ya sukari ambayo ni nyepesi kabisa kutumika mwilini, na madaktari wamevumbua karibu kuwa glucose ina faida kutibu maradhi mengi, kwa kupiga sindano, na kwa mdomo na kwa nyuma, kwa kuwa inatia nguvu, na inapinga sumu ya maadeni kadhaa wa kadhaa, na sumu inayo patikana kwa maradhi ya viungo, kama kuingia sumu kwa mkojo na maradhi ya kuwa manjano jaundice na mengineyo. Vile vile imethibiti kuwa Vitamin nyingi hupatikana humo, na khasa Vitamin B complex.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha kuleni katika kila tunda mnalolipenda na mzifuate njia za Mola wenu mlizotayarishiwa ili kutafuta riziki majabalini na kati ya miti. Na Allah Mtukufu Amewasahilishia njia hizo, hampotei katika kurudi hata kama ni mbali. Inatoka kwenye matumbo ya nyuki asali yenye rangi tafauti: nyeupe, manjano, nyekundu na nyiginezo. Na kwenye hiyo asali pana tiba ya magonjwa ya watu. Hakika katika hayo wanayoyafanya nyuki pana ushahidi wenye nguvu juu ya uwezo wa Muumba wao kwa watu wanaofikiria na wakazingatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net