An-Nahl 16:57
النحلوَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ ٱلْبَنَـٰتِ سُبْحَـٰنَهُۥ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ
Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu mabinti, Subhanahu (ametakasika)! Na wao wenyewe, ati ndiyo wana hayo wanayoyatamani!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliyetakasika! Na wao wenyewe, ati ndio wawe na hayo wanayo yatamani! [57]
[57] Na hujaalia kumpa Mwenyezi Mungu yale wayachukiayo wao, kwa kudai kuwa Malaika ni watoto wake wa kike, na wao wanawaabudu. Mwenyezi Mungu apishe mbali na hayo! Na wao ati wanajipa wayapendayo nayo ni watoto wanaume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na makafiri wanamsingizia Allah Mtukufu kuwa ana watoto wa kike na huwa wakisema, «Malaika ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu». Ametakasika Allah Mtukufu na neno lao. Na wanajichukulia wao wenyewe watoto wa kiume wanaowapenda.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net