An-Nahl 16:35
النحلوَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ نَّحْنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ
Na washirikina walisema: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharamisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo, walifanya wale waliokuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na washirikina wanasema: Mwenyezi Mungu angeli taka tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeli harimisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo walifanya walio kuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipo kuwa kubalighisha kwa uwazi? [35]
[35] Na washirikina wakasema kwa inda na ukosefu: Lau kama Mwenyezi Mungu angeli penda tumuabudu Yeye tu peke yake na tumt'ii kwa anayo tuamuru, basi tusingeli muabudu mwenginewe, wala tusingeli harimisha sisi wenyewe kitu asicho harimisha Yeye kama Bahira na Saiba. Na hii ni hoja potovu wanayo itafutia njia katika ukafiri wao. Na makafiri walio kwisha tangulia walitoa hoja kama hizo, baada ya kuwapelekea Mitume wetu, wakaamrisha Tawhidi (kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja), na kumt'ii Yeye, na wakawakataza ushirikina na kuharimisha asivyo harimisha Mwenyezi Mungu. Hoja ikasimama dhidi yao. Na Mitume wetu wakatimiza tuliyo waamrisha wayafikishe. Na juu yetu kuwahisabu wao. Na Mitume hawana jukumu zaidi ya hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na washirikina walisema, «Lau Allah Mtukufu Angetaka tumuabudu Yeye Peke Yake, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye, sisi wala baba zetu kabla yetu, wala hatungaliharamisha chochote Asichokiharamisha». Ni hoja kama hizi za kipotofu walizozitumia makafiri waliopita. Na wao ni warongo, kwani Allah Mtukufu Aliwaamrisha na Akawakataza na Akawawezesha kuyasimamia Aliyowakalifisha nayo, na Akawapa nguvu na matakwa yanayotokana na vitendo vyao. Kwa hivyo, kujenga hoja kwao wakitegemea mapitisho ya Allah Mtukufu na makadirio Yake ni ubatilifu mkubwa baada ya kuonywa kwao na Mitume. Na Mitume wenye kuwaonya hawana la zaidi isipokuwa kuufikisha ujumbe ulio wazi waliokalifishwa nao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net