An-Nahl 16:24
النحلوَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوٓا۟ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Na wanapoambiwa, "Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?" Husema: Hadithi za kubuni za wa mwanzo!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo ambiwa: Kateremsha nini Mola wenu Mlezi? Husema: Hadithi za kubuni za watu wa kale! [24]
[24] Na wakiulizwa hao makafiri wanao jivuna: Mola wenu Mlezi kamteremshia nini Muhammad? Wao hujibu kwa inda: Hayo anayo dai kuwa Mwenyezi Mungu kamteremshia si chochote ila uzushi na upuuzi walio tunga watu wa zamani naye akayanukulu na akawa anayakariri tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi wanapoulizwa, hawa washirikina, kuhusu yale aliyoteremshiwa Nabii Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, wanasema kwa urongo na uzushi, «Hakuleta isipokuwa visa vya waliotangulia na porojo zao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net