Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 15 · Aya ya 98

Al-Hijr 15:98

الحجر

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ

Maana

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanaomsujudia. [98]

[98] Ikikupata dhiki hiyo mkimbilie Mwenyezi Mungu Mtukufu umwelekee, na umt'ii na umnyenyekee, na utake msaada kwa Sala, kwani humo ndio imo poza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kimbilia kwa Mola wako pindi unaponyongeka moyo wako, na mtakasie yeye kwa kumshukuru na kumsifu. Na uwe ni miongoni mwa wenye kuswali kwa ajili ya Allah Mtukufu na wenye kumuabudu, kwani kwa kweli hilo litakutosheleza na lile lenye kukutia kero.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hijr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net