Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 15 · Aya ya 90

Al-Hijr 15:90

الحجر

كَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٱلْمُقْتَسِمِينَ

Maana

Kama hivyo tuliwateremshia waliogawa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa, [90]

[90] Haya ni kama maonyo ya walio igawanya Qur'ani wakaifanya ati ni mashairi, na ukohani, na hadithi za kale na mengineyo. Nao wasiiamini juu ya kusimama hoja juu yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ni mwenye kuwaonya nyinyi isije ikawapata adhabu kama ile Aliyoiteremsha Allah Mtukufu kwa wale walioigawanya Qur՚ani, wakaiamini baadhi yake na wakaikanusha baadhi nyingine miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara na makafiri wa Kikureshi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hijr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net