Al-Hijr 15:81
الحجروَءَاتَيْنَـٰهُمْ ءَايَـٰتِنَا فَكَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ
Na tuliwaletea ishara zetu, nao wakawa wanazipa migongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza. [81]
[81] Tuliwabainishia hoja zenye kuonyesha uwezo wetu, na Utume wa Mtume wetu, nao wakayapuuza, wala wasiyafikiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwapa watu wa Ṣãliḥ aya zetu zinazojulisha usahihi wa mambo ya haki ambayo amekuja nayo kwao Mtume Ṣãliḥ, na miongoni mwayo ni ngamia, wazingatie kwa aya hizo na wakawa ni wenye kujiweka mbali nazo na kuzipa mgongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net