Al-Hijr 15:79
الحجرفَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na hakika miji miwili hii iko kwenye njia iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia iliowazi. [79]
[79] Tukawateremshia nakama yetu. Na mabaki yao yapo njiani yanaonekana, na mpita njia akiwa ni mtu wa Imani basi anaweza kuzingatia kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivyo basi tuliwaadhibu kwa mtetemeko na adhabu ya siku ya uvuli. Na kwa hakika, makazi ya watu wa Lût na watu wa Shu‛ayb yako katika njia iliyo wazi, watu wanayapitia katika safari zao na wanapata mazingatio.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net