Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 15 · Aya ya 72

Al-Hijr 15:72

الحجر

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِى سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ

Maana

Ninaapa kwa uhai wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. [72]

[72] Ewe Nabii Muaminifu! Naapa kwa haki ya uhai wako! Hawa wamo katika mghafala, hawajui yatakayo wateremkia. Wamekuwa kama walio lewa! Hakika wao wamo katika upotovu, wanatapatapa, hawajui wapite wapi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Muumba Anaapa kwa Anayemtaka na kwa Anachokitaka. Ama muumbwa haifai kwake kuapa isipokuwa kwa jina la Allah Mtukufu. Na Ameapa Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa uhai wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kumtukuza kwa watu, kwamba watu wa Lût wako kwenye upotevu mkali, wana shaka na wako kwenye ushindani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hijr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net