Al-Hijr 15:69
الحجروَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. [69]
[69] Na mwogopeni Mwenyezi Mungu Mtukufu! Msifanye uchafu wenu, mkanipatisha hizaya na madhila mbele yao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na yaogopeni mateso ya Allah Mtukufu, wala msiwasumbue mkaniingiza kwenye unyonge na madharau kwa kuwaudhi wageni wangu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net