Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 15 · Aya ya 60

Al-Hijr 15:60

الحجر

إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ قَدَّرْنَآ ۙ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ

Maana

Isipokuwa mkewe. Tumekwishapitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni mwa watakaosalia nyuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma. [60]

[60] Na hatoangamia katika ahli zake ila mkewe, kwani yeye hakumfuata mumewe, bali yu pamoja na hao wakosefu ambao wanao stahiki adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ama yule mke wake aliye kafiri, tumepitisha kwa amri ya Allah Mtukufu kumwangamiza pamoja na watakaosalia kwenye adhabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hijr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net