Al-Hijr 15:29
الحجرفَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَـٰجِدِينَ
Basi nitakapomtengeneza sawasawa, na nikampulizia katika roho yangu, basi angukeni kumsujudia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. [29]
[29] Nikisha kamilisha kumuumba, na nikampulizia roho ambayo ninaimiliki, basi teremkeni kwa nyuso zenu mkimsujudia, kwa kumwamkia na kumhishimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi nitakapomtengeneza na kulikamilisha umbo lake na nikapuliza roho ndani yake, mwangukieni hali ya kusujudu, sijida ya maamkizi na heshima na si sijida ya ibada.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net