Al-Hijr 15:26
الحجروَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِن صَلْصَـٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
Na hakika tulimuumba Mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. [26]
[26] Na Sisi katika kuumba kwetu walimwengu katika dunia hii, tumeumba namna mbili - Tumemuumba mtu kwa udongo mkavu wenye kutoa sauti ukigongwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika tulimuumba Ãdam kwa udongo mkavu, ukigongwa unasikiwa sauti. Na udongo huu mkavu ni miongoni mwa udongo mweusi uliogeuka rangi yake na harufu yake kwa kipindi kirefu cha kukaa kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net