Al-Hijr 15:17
الحجروَحَفِظْنَـٰهَا مِن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ رَّجِيمٍ
Na tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye. [17]
[17] Lakini Sisi tumezihifadhi na kila shetani anaye stahiki kupigwa vimondo na kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumeuhifadhi uwingu huo na kila Shetani Aliyetolewa na aliyefukuzwa kutoka kwenye rehema za Allah Mtukufu ili asiufikie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net