Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 15 · Aya ya 12

Al-Hijr 15:12

الحجر

كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُۥ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Na kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza katika nyoyo za wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu. [12]

[12] Kama tulivyo itia Qur'ani katika nyoyo za Waumini ikaingiza mwangaza, basi kadhaalika tumeingiza upotovu katika nyoyo za walio pigwa muhuri wa ukosefu; hali ya katika nyoyo zao ikawa kinyume cha hayo. Upotovu ukatia mizizi katika roho zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kama tulivyoutia ukafiri kwenye nyoyo za ummah waliotangulia kwa sababu ya kuwafanyia shere Mitume na kuwakanusha, hivyo ndivyo tunavyofanya kwenye nyoyo za washirikina miongoni mwa watu wako waliofanya uhalifu wa kumkanusha Allah Mtukufu na kuwakanusha Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hijr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net