Al-Hijr 15:1
الحجرالٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ وَقُرْءَانٍ مُّبِينٍ
Alif Lam Ra.[1] Hizi ni Aya za Kitabu na Qur-ani inayobainisha.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alif Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha. [1]
[1] Hizi ni Aya za Kitabu cha kusomwa, chenye kubainisha, chenye kuweke wazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
(Alif, Lâm, Râ) Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa. hizo ni aya tukufu miongoni mwa aya za Kitabu kitukufu kilichoteremshwa kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Nazo ni aya za Qur’ani zenye kufafanua kweli kwa matamko mazuri zaidi na yaliyo wazi zaidi na yenye kuonyesha zaidi makusudio. Kitabu na Qur’ani ni kitu kimoja; na hapa Allah Mtukufu Ameyakusanya pamoja majina mawili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net