Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 6

Ibrahim 14:6

ابراهيم

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ أَنجَىٰكُم مِّنْ ءَالِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوٓءَ ٱلْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبْنَآءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَآءَكُمْ ۚ وَفِى ذَٰلِكُم بَلَآءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ

Maana

Na Musa alipowaambia kaumu yake, "Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu pale alipowaokoa kutokana na watu wa Firauni waliokuwa wakiwatia adhabu mbaya kabisa, wakiwachinja wana wenu wanaume, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unaotoka kwa Mola wenu Mlezi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Musa alipo waambia watu wake: Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kujaalieni, pale alipo kuokoeni kutokana na watu wa Firauni walio kupeni adhabu mbaya kabisa, wakiwachinja wenenu wanaume, na wakiwawacha hai wanawake. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unao toka kwa Mola wenu Mlezi. [6]

[6] Ewe Nabii! Wakumbushe watu wako, huenda wakazingatia, wakati Musa alipo waambia watu wake kwa kufuata amri ya Mola wako Mlezi: Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu, pale alipo kuvueni kutokana na kaumu ya Firauni, nao wakikupatilizeni kwa adhabu ovu kabisa. Wakikufanyisheni kazi ngumu, wakiwachinja watoto wenu wa kiume, na wakiwaacha wa kike na kuwaweka katika unyonge na udhalili bila ya kuwauwa. Na mateso yote yaliyo tajwa na kuokoka ni mtihani mkubwa unao toka kwa Mwenyezi Mungu, ili upate kudhihiri uwezo wa kusubiri na kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, kisa cha Mûsâ pindi alipowaambia watu wake, «Kumbukeni neema ya Allah Mtukufu kwenu alipowaokoa kutokana na Fir‛awn na wafuasi wake waliokuwa wakiwaonjesha adhabu kali zaidi, wakiwaua watoto wenu wa kiume, ili asitokee kati yao atakayeuvamia ufalme wa Fir‛awn, na walikuwa wakiwaacha wanawake wenu kwa kutumika na kudharauliwa. Na katika misukosuko hiyo na kuokolewa huko ni mtihani mkubwa utokao kwa Mola wenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net