Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 49

Ibrahim 14:49

ابراهيم

وَتَرَى ٱلْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُّقَرَّنِينَ فِى ٱلْأَصْفَادِ

Maana

Na utaona wahalifu siku hiyo wamefungwa pamoja katika minyororo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na utaona wakhalifu siku hiyo wamefungwa katika minyororo; [49]

[49] Utawaona makafiri Siku ya Kiyama wamefungwa pingu pamoja na mashetani wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na utawaona,ewe Nabii, waasi Siku ya Kiyama wamefungwa pingu, mikono yao miguu yao imekutanishwa pamoja kwa minyonyoro, na hali wakiwa watwevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net