Ibrahim 14:41
ابراهيمرَبَّنَا ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ ٱلْحِسَابُ
Mola wetu Mlezi! Nisamehe mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku itakaposimama hesabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. [41]
[41] Ewe Mola wetu Mlezi! Nisamehe madhambi yaliyo niponyoka, na wasamehe wazazi wangu, na Waumini wote, Siku itapo hakikishwa hisabu, na baadae ikawa malipo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Ewe Mola wetu! Nisamehe iwapo yametokea kutoka kwangu mambo ambayo binadamu hawasalimiki nayo, na uwasamehe wazazi wangu wawili (Hapa ni kabla haijamfunukia kwamba baba yake ni adui wa Allah Mtukufu) na uwasamehe Waumini wote Siku ambayo watu watasimama kuhesabiwa na kulipwa»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net