Ibrahim 14:36
ابراهيمرَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ ٱلنَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِى فَإِنَّهُۥ مِنِّى ۖ وَمَنْ عَصَانِى فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza wengi wa watu. Basi aliyenifuata mimi, huyo hakika ni miongoni mwangu. Na aliyeniasi, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza watu wengi. Basi aliye nifuata mimi huyo ni wangu, na aliye niasi, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [36]
[36] Kwani masanamu yamepelekea kupotea watu wengi kwa kuyaabudu. Basi katika dhuriya zangu, wenye kunifuata mimi na wakakuabudu Wewe kwa ikhlasi, basi hao ni watu wa Dini yangu. Na wenye kuniasi kwa kushika ushirikina, basi Wewe ni Muweza wa kuwaongoa, kwani Wewe ni Mwingi wa maghfira na rehema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Mola wangu! Masanamu yamesababisha kuwaepusha watu wengi na njia ya ukweli. Basi mwenye kunifuata mimi katika kumpwekesha Allah Mtukufu, yeye atakuwa kwenye Dini yangu na mwendo wangu, na mwenye kwenda kinyume na mimi, katika mambo ambayo si ya ushirikina, basi wewe ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kufanya madhambi, kwa fadhila zako, ni Mwingi wa huruma kwao, unamsamehe unayemtaka miongoni mwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net