Ibrahim 14:31
ابراهيمقُل لِّعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يُقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خِلَـٰلٌ
Waambie waja wangu walioamini, wadumishe Swala, na watoe katika tulivyowaruzuku, kwa siri na dhahiri, kabla ya kufika kwa Siku isiyokuwa na biashara yoyote wala urafiki wa dhati.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waambie waja wangu walio amini, washike Swala, na watoe katika tulivyo waruzuku, kwa siri na dhaahiri, kabla haijafika Siku isiyo kuwa na biashara wala urafiki. [31]
[31] Ewe Muhammad! Waambie waja wangu walio sadiki, wakaamini, na wakatenda mema: Shikeni Swala, na toeni baadhi ya tuliyo kuruzukuni katika njia za kheri, kwa siri na kwa dhaahiri, kabla ya kufika siku ambayo haifai kitu kupatana kibiashara wala hisani ya urafiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, waja wangu walioamini watekeleze Swala kwa namna yake inayotakikana na watoe sehemu ya mali tuliyowapa katika njia za heri, za lazima na zinazopendekezwa, watoe kwa siri au waziwazi, kabla ya kuja Siku ya Kiyama ambayo haitafaa kitu fidia wala urafiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net