Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 12

Ibrahim 14:12

ابراهيم

وَمَا لَنَآ أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى ٱللَّهِ وَقَدْ هَدَىٰنَا سُبُلَنَا ۚ وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَآ ءَاذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُتَوَكِّلُونَ

Maana

Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye njia zetu. Na hakuna hakika tutayavumilia hayo maudhi mnayotuudhi nayo. Na juu ya Mwenyezi Mungu na wategemee wanaotegemea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye Njia zetu. Na hapana shaka sisi tutayavumilia hayo maudhi mnayo tuudhi. Na juu ya Mwenyezi Mungu wategemee wanao tegemea. [12]

[12] Na sisi tuna udhuru gani wa kuacha kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye aliye tuongoza kila mmoja wetu kwenye njia yake na maelekeo yake aliyo mwekea, na akamlazimisha afuate katika Dini? Na hakika sisi tunatilia mkazo tegemeo letu kwa Mwenyezi Mungu; na hapana shaka tutayavumilia maudhi yenu ya inadi na kutaka miujiza. Na juu ya Mwenyezi Mungu peke yake ndio humtegemea wanao tegemea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Na vipi sisi tusimtegemee Allah Mtukufu, na hali Yeye Ndiye Aliyetuongoza njia ya kuokoka na adhabu Yake kwa kufuata hukumu za dini Yake? Na sisi tutavumilia sana makero yenu kwetu kwa maneno maovu na mengineyo. Na kwa Allah Mtukufu Peke Yake ni lazima Waumini wamtegemee Awapatie nusura na ushindi juu ya maadui zao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net