Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 3

Yusuf 12:3

يوسف

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ ٱلْقَصَصِ بِمَآ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِۦ لَمِنَ ٱلْغَـٰفِلِينَ

Maana

Sisi tunakusimulia simulizi nzuri zaidi kwa kukufunulia Qur-ani hii. Na ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa walioghafilika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua. [3]

[3] Sisi tunakusimulia, ewe Nabii, visa vizuri kabisa kwa kukufunulia Kitabu hichi. Na kabla ya haya ulikuwa umeghafilika nayo, huyajui, haya, wala mawaidha yaliomo ndani yake, na Aya zake zilizo wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sisi tunakusimulia wewe, ewe Mtume, visa vizuri zaidi kwa wahyi tuliyokuletea wa hii Qur’ani, na ingawa, kabla ya kukuteremshia, ulikuwa ni miongoni mwa walioghafilika nazo, hujui chochote kuhusu habari hizi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net